MASOMO YA MISA 3 DISEMBA 2017 JUMAPILI YA KWANZA YA MAJILIO MWAKA B WA KANISA

MWANZO:

Zab. 25:1 – 3
Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu, nimekutumaini wewe, nisiaibike, adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja.

SOMO 1:Isa.2:1-5


Hili ni neon aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu. Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; maana katika Sayuni itatoka sheshariaa neon la Bwana katika Yerusalemu.
Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa linguine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 122:1 – 4, 8 – 9  (K) 1

(K) Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.

Nalifurahi waliponiambia,
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama,
Ndani ya malango yako Ee Yerusalemu. (K)

Ee Yerusalemu uliyejengwa,
Kama mji ulioshikamana;
Huko ndiko walikopanda kabila,
Kabila za Bwana. (K)

Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu
Niseme sasa, Amani ikae nawe.
Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu,
Nikutafutie mema. (K)

SOMO 2:Rum.13:11-14


Ndugu zangu, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia; basin a tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kw augomvi na wivu. Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.

Neon la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Zab. 85:7

Aleluya, aleluya,
Ee Bwana utuonyeshe rehema zako, utupe na wokovu wako.
Aleluya.

INJILI:Mt.24:37-44


Siku ile, Yesu aliwaambia wafuasi wake kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.


No comments:

Powered by Blogger.