MASOMO YA KUMBUKUMBU YA WATAKATIFU MALAIKA WALINZI 2 OCTOBA 2017

SOMO 1:Zek.9:1-8

Neno la Bwana wa majeshi likanijia,  kusema,
 ''Bwana wa majeshi asema hivi:
Mimi ninawivu kwa ajili ya Sayuni, wivu mkuu,
nami nina wivu kwa ajili yake kwa ghadhabu kuu.
Bwana asema hivi:
Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa,  Mji wa kweli,
na mlima wa Bwana wa Majeshi utaitwa, Mlima mtakatifu.
Bwana wa majeshi asema hivi:
Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu anamkongojo wake mkononi,
kwa kuwa ni mzee sana.
Na hizo njia zitajaa wavulana na wasichana, wakicheza katika njia zake.
   Bwana wa majeshi asema hivi:
Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je,  liwe neno gumu mbele ya macho yangu?
Asema Bwana wa Majeshi.
Bwana wa majeshi asema hivi:
Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi; nami nitawaleta, nao  watakaa katikati ya Yerusalemu;
nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki.


WIMBO WA KATIKATI
Zab. 102:15-20, 28, 21-22

(K) Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, atakapoonekana katika utukufu wake.

Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana,
na wafalme wote wa dunia  utukufu wako:
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, atakapoonekana katika utukufu wake.
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,  asiyadharau maombi yao.(K)

Kizazi kitakapokuja kitaandikiwa hayo, na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi, ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, na kuwafungua walioandikiwa kufa.(K)

Wana wa watumishi wako watakaa, na wazao wao wataimarishwa mbele zako.
Watu watalitangaza jina la Bwana katika Sayuni, na sifa zake katika Yerusalemu,
pindi mataifa watakapo kusanyika pamoja, falme nazo ili kumtumikia Bwana.(K)


INJILI:Lk.9:46-50


Wanafunzi walianza kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa mwiongoni mwao, Naye Yesu alipotambua mawazo  ya mioyo yao, alitwaa mtoto mdogo akamweka karibu naye,  akawaambia,   ''Yeyote  atakayempokea  mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi;  na yeyote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa. "

   Yohane akajibu akamwambia,  ''Bwana mkubwa,  tuliona mtu anatoa pepo kwa jina lako; tukamkataza, kwa sababu hafuatani na sisi. Yesu akamwambia,  '' Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.

Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.

No comments:

Powered by Blogger.