MASOMO KUMBUKUMBU YA BIKIRA MARIA MT.WA ROZARI JUMAMOSI 7 OCTOBA 2017
SOMO 1.Bar.4:5-12,27-29
Jipeni moyo watu wangu,Israeli mnaokumbukwa!Mliuzwa kwa mataifa lakini hamkuangamia.Kwa kuwa mlimtia Mungu ghadhabu mlitolewa kwa adui zenu;Mlimwasi yeye aliyewaumba,mkitoa sadaka kwa pepo,si kwa Mung;mlisahau Mungu wa milele aliyewalea,na Yerusalemu mama yenu.Huyu mama aliiona ghadhabu ya Mungu iliyo juu yenu,akasema:Enyi wa Sayuni,sikilizeni!Mungu ameleta juu yangu huzuni kubwa.Nimeuona utumwa wa wanangu ambao Aliye wa milele amewapatiliza.Kwa furaha naliwalea;bali kwa kilio na maombolezo naliwaaga.Asisimange juu yangu mtu yeyote,mimi niliye mjane na kuachwa na watu.Kwa sababu ya dhambi ya wanangu nimeachwa ukiwa,kwa kuwa walikengeuka na kuiacha sheria ya Mungu.Jipeni moyo,wanangu,mlilieni Mungu!Maana yeye aliyewapatiliza mambo haya atawakumbuka.Kama ilivyokuwa nia yenu kumwasi Mungu,rudini sasa,mtafuteni mara kumi zaidi;maana yeye aliyeyaleta mapigo haya juu yenu atawarudishia Furaha ya milele pamoja na wokovu wenu.
K:Bwana husikia wahitaji.-Zab.69:32-36
INJILI:Lk.10:17-24
Wale sabini waliporudi kwa furaha,wakisema,Bwana,hata pepo wanakutii kwa jina lako.Akawaambia,Nilimwona shetani,akianguka kutoka mbinguni kama umeme.Tazama,nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge,na nguvu zote za yule adui,wala hakuna kitu kitakachowadhuru.Lakini,msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii;bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu,akasema,Nashukuru,Baba,Bwana wa mbingu na nchi,kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili;umewafunulia watoto wachanga;Naam,Baba,kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza.Akasema,Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu,wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba;wala amjuaye baba ila mwana,na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.Akageukia wanafunzi wake,akasema nao kwa faragha,Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone;na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.

No comments: