MASOMO JUMA LA 22 LA MWAKA 7 SEPTEMBA 2017
SOMO1:Kol.1:9-14
Tangu siku tuliposikia habari yenu,hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu,ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana,mkimpendeza kabisa;mkizaa matunda kwa kila kazi njema,na kuzidi katika maarifa ya Mungu;mkiwezeshwa kwa uwezo wote,kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake,mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;mkishukuru Baba aliyewastailisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.Naye alituokoa katika nguvu za giza,atakuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;ambaye katika yeye tuna ukombozi,yaani msamaha wa dhambi.
K:Bwana ameufunua wokovu wake.-Zab.98:2-6
INJILI:Lk.5:1-11
Makutano walipomsonga Yesu walisikiliza neno la Mungu,Yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa,lakini wavuvi wametoka,wanaosha nyavu zao.Akaingia katika chombo kimoja,ndicho chake Simoni,akimtaka akipeleke mbali kidogo hadi pwani.Akaketi,akawafundisha makutano ali chomboni.Hata alipokwisha kunena,alimwambia Simoni,Tweka mpaka kilindini,mkaushushe nyavu zenu mvue samaki.Simoni akajibu akamwambia,Bwana mkubwa,tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha,tusipate kitu;lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.Basi,walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno,nyavu zao zikaanza kukatika;wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili,waje kuwasaidia;wakaja,wakavijaza vyombo vyote viwili,hata vikataka kuzama.Simoni Petro alipoona hayo,alianguka magotini pa Yesu,akisema,Ondoka kwangu,kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi,Bwana.Maana alishikwa na ushangao,yeye na wote waliokuwa pamoja naye,kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;na kadhalika Yakobo na Yohane,wana wa Zebedayo,waliokuwa washirika wa Simoni.Yesu akamwambia Simoni,Usiogope,tangu sasa utakuwa ukivua watu.Hata walipokwisha kuviegesha pwana vyombo vyao,wakaacha vyote wakamfuata.

No comments: