MASOMO YA LEO IJUMAA 21 JULY,2017 JUMA LA 15 LA MWAKA

SOMO1:Kut.11:10-12:13

Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao;Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu,asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.Bwana akanena na Musa na Haruna katika nchi ya Misri,akawaambia,mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu.Semeni na mkutano wote wa kwanza wa mwaka kwenu.Semeni na mkutano wote wa Israeli,mkawaambie siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo kwa hesabu ya nyumba ya baba zao,mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana -kondoo,basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba uake na watwae mwana-kondoo mmoja,kwa kadiri ya hesabu ya watu;kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu,ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila,mume wa mwaka mmoja;mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi uleule;nakusanyiko lote la mkutano wa Israli watamchinja jioni.Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kutia katika miimo,miwili na katika kizingiti cha juu,katika zile nyumba watakazomla.Watakula nyama ya usiku uleule,imeokwa motoni,pamoja na mkate usiotiwa chachu;tena pamoja na mboga zenye uchungu.Msiile mbichi,wala ya kutokoswa majini,bali imeokwa motoni;kichwa chake pamoja na miguu yake na nyama zake za ndani.Wala msisase kitu chake chochote hata asubuhi,bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.Tena mtamla hivi;mtakuwa mmefungwa viuno vyenu,mmevaa viatu vyenu miguuni,na fimbo zenu mikononi mwenu,nanyi mtamla kwa haraka;ni pasaka ya Bwana.Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo,nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri,wa mwanadamu na wa mnyama;nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri;mimi ndimi Bwana.Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwemo;nami nitakapoina ile damu,nitapita juu yenu,lisiwapate pigo lolote likawaharibu,nitakapoipiga nchi ya Misri.Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu,nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana;mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote,kwa amri ya milele.

K:Nitakipokea kikombe cha wokovu,na kulitangaza jina la bwana.-Zab.116:12-13,15-18.

INJILI:Mt.12:1-8

Wakati ule yesu alipita katika mashamba siku ya sabato,wanafunzi wake wakaona njaa,wakaanza kuvunja masuke,wakala,na Mafarisayo walipowaona,walimwambia,Tazama!wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.Akawaambia,Hamkusoma alivyotenda Daudi,alipokuwa na njaa,yeye na wenziwe?Jinsi alivyoingia katika ya Mungu akaila mikate ile ya wonyesho,ambayo si halali kwake kuila wala kwa wenziwe,ila kwa makuhani pekee yao?Wala hamkusoma katika torati,kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?Lakini nawaambieni,kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.Lakini kama mngalijua maana ya maneno haya,Nataka rehema,wala si sadaka,msingaliwalaumu wasio na hatia.Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

No comments:

Powered by Blogger.