MASOMO YA LEO ALHAMISI JUMA LA 15 LA MWAKA

SOMO1:Kut.3:13-20

Musa alimwambia Mungi,Tazama,nitakapofika kwa wana wa Israeli,na kuwaambia,Mungu wa baba zenu amenituma kwenu;nao wakaniuliza,jina lake ni nani?Niwaambie nini?Mungu akamwambia Musa,Mimi niko ambaye niko;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israel;Mimi niko amenituma kwenu.Tena Mungu akamwambia Musa ,waambie wana wa Israel maneno haya,Bwana mungu wa baba zenu,Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka,Mungu wa Yakobo,amenituma kwenu;hili ndilo jina langu hata milele,nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.Enenda,ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja,ukawaambie,Bwana mungu wa baba zenu,Mungu wa Yakobo,amenitokea,akaniambia,Hakika nimewajilieni,tenanimeyaona mnayotendewa huko Misri;nami nikasema,nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani,na Mrihi,na Mwamori,na Mperizi,na Mhivi na Myebusi,nchi ijaayo maziwa na asali.Nao watakusikia sauti yako;nawe utakwenda,wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa misri,na kuwaambia,Bwana Mungu wa Waebrania,amekutana nasi;basi sasa twakuomba,tupe ruhusa twende mwendo wa siku tatu jangwani,ili tumtolee dhabihu bwana,Mungu wetu.Nami najua ya kuwa huyo Mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu,la,hata kwa mkono wa nguvu.Nami nitaunyosha mkono wangu,na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote,nitakazofanya kati yake,kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.

K:Bwana analikumbuka agano lake milele.-Zab.105:1,5,8-9,24-27.

INJILI:Mt.11:28-30

Yesu aliwaambia makutano:Njoni kwangu,ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu,mjifunze kwangu;kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo;nanyi mtapata raha nafsini mwenu;maana nira yangu ni laini,na mzigo wangu ni mwepesi.

No comments:

Powered by Blogger.