MASOMO YA JUMA LA 14 LA MWAKA

Somo 1:Mwa.41:55-57;42:5-7,17-24
Nchi yote ya Misri ilipoona njaa,watu walimlilia Farao awape chakula.Farao akawambia Wamisri wote Enendeni kwa Yusufu;atakavyowaambia,fanyeni.Njaa ikawa katka dunia yote pia.Yusufu akazifungua ghala zote,akawauliza Wamisri.Njaa ikawa nzito Katika nchi ya Misiri.Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu;ili wanunue nafaka;njaa imekuwa nzito katika dunia yote.Wana wa Israeli wakaja wanunue chakula,miongoni mwao walikuja, kwa kuwa kulikuwa na njaa katika nchi ya kaanani.Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi,ndiye aliyewauzia watu wote ww nchi.Nao ndugu zake Yusufu wakaja,wakainama kifudifudi mbele yake.Yusufu akawaona nduguze,akawatambua,lakini alijifanya kama mgeni kwao.Akasema nao kwa maneno makali,akawaambia,Mmetoka wapi ninyi? Wakasema,tumetoka nchi ya kaanani ili tununue chakula.Akawatia wote gerezani siku tatu.Yusufu akawaambia siku ya tatu,Fanyeni hivi,mkaishi,maana mimi namcha Mungu.Kama ni wa kweli ninyi,ndugu yenu mmoja na afungwe gerezani,nanyi nendeni mkachukue nafaka kwa njaa ya nyumba zenu,mkalete ndugu yenu mdogo kwangu;hivyo maneno yenu yatahakikishwa,wala hamtakufa.Ndivyo walivyofanya.Wakaambiana,kweli,sisi tulimkosa ndugu yetu kwa kuwa tuliona shida ya roho yake,alipotusihi,walahatukusikia;kwahiyo shida hii imetupata.Reubeni akajibu akawaambia,Sikuwaambia,nikisema,msimkose kijana?Wala hamkusikia;kwahiyo damu yake inatakwa tena.Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia,kwasababu alikuwapo mkalimani kati yao.Akajitenga nao akalia.Kisha akawarudia,na kusema nao,akamtwaa Simeoni miongoni mwao,akamfunga mbele ya macho yao.

K:Ee Bwana fadhili zako zikae nasi,kama vile ulivyotungoja Wewe.-Zab.33:1-2,10-11,18-19

Injili:Mt.10:1-7
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili,akawapa amri juu ya pepo wachafu,wawatoe,na kuwapoza magonjwa yote ya udhaifu na wa kila aina.Na majina yao mitume kumi na wawili ni haya;Wakwanza Simoni aliyeitwa Petro,na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo,na Yohane nduguye;Filipo,na Bartholomayo;Tomaso,na Mathayo mtoza ushuru;Yakobo wa Alfayo,na Thadayo;Simoni Mkananayo,na Yuda Iskariote,naye ndiye mwenye kumsaliti.Hao Thenashara Yesu aliwatuma,akawaagiza,akisema.Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.Na katika kuenenda kwenu,hubirini,mkisema,Ufalme wa mbinguni umekaribia.

No comments:

Powered by Blogger.