MASOMO YA MISA,5 SEPTEMBA 2018 JUMATANO JUMA LA 22 LA MWAKA WA KANISA.

SOMO 1:1Kor.3;1-9

Ndugu zangu, mimi siwezi kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?
Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jingo la Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 33:12 – 15, 20 – 21 (K) 12

(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.

Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia. (K)

Toka mahali pake aketipo
Huwaangalia wote wakaao duniani.
Yeye aiumbaye mioyo yao wote
Huzifikiri kazi zao zote. (K)

Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Maana mioyo yenu itamfurahia,
Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu. (K)

SHANGILIO
Yak. 1:21

Aleluya, aleluya,
Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.

INJILI:Lk.4:38-44

Yesu alitoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni, mamaye mwomba kwa ajili yake. Akasimama karibu naye, akikemea ile hma, ikamwacha; mara hiyo akaondoka, akawatumikia.
Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya. Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelel na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.
Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafutatafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao. Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

No comments:

Powered by Blogger.