MAPADRI WALIOPADRISHWA JULAI 7 2018 WA JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM KATIKA VIWANJA VYA MSIMBAZI


Mapdri waliopadrishwa 07,July.2018

kutokea kushoto ni Pd. Edes Rufin - Paroko

Msaidizi Parokia ya Kibaha & Msimamizi wa Shule ya Yohane Bosco Kibaha.

Pd. Ernest Boyo - Paroko Msaidizi Kanisa Kuu la Mt. Joseph.

Pd. John Mallya - Paroko Msaidizi Parokia ya Kijichi.

Cyprino Kikoti SDS - Paroko Msaidizi Parokia ya Mt. Maurus Kurasini.

Pd. Exuper Mkwawe SDS - Paroko Msaidizi Parokia ya Sinza.

Pd. Pascal Mapendo

Pd. Raymond Makhatya

....Nitume mimi Bwana...

Katika Misa ya Upadrisho 07,July.2018 Baba

 Mwadhama aliwakabidhi Mapadri Sala ya

kuweza kujiombea. Pia alitoa wito kwa

Mapadri wa zamani pia kuendelea kusali

sala hiyo isemayo: "Ee Yesu Mwema

unifanye niwe Kuhani kulingana na

Mapenzi ya Moyo wako."

Tuiombee miito mitakatifu.


        Pia katika misa hiyo ya Upadilisho

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alitoa
maelezo juu ya Askofu mwandamizi YUDA

THADAI RUWAI'CHI aliyeteuliwa na Baba

Mtakatifu Papa Fransis.

"Wote mmekwisha kusikia kwamba

tumepata Askofu Mwandamizi katika jimbo kuu la Dar es salaam.Askofu Mkuu Yuda

Thadeus Rwaichi tunatarajia apokelewe hapa jimboni 07 septemba 2018."

Alisisitiza na kusema kupokelewa kwa

Askofu Mwandamizi katika jimbo

aliloteuliwa kunategemea Mambo
yafuatayo;

1. Baba Mtakatifu awe ameleta hati yake ya  kumteua kuwa Askofu Mwandamizi.

2. Yeye Mwenyewe atapoona yupo tayari kutoka kule Mwanza awe ameweka vitu vinavyotakiwa halafu aje hapa kwetu.

Baba Mwadhama alisema:

"Iwapo itatokea kitu fulani hapa katikati

labda anaomba amalizie kitu fulani kule Mwanza au hati ya Baba Mtakatifu

imechelewa kufika, tutabadilisha tarehe kulingana na utayari huo.

Baba Mwadhama alitoa tamko kwa

Mapadri mbalimbali ambao wameanza kumtaja Baba Askofu Mwandamizi katika

sala ya Ekaristi naye alisema;

"Sasa nimepita katika Parokia Mbalimbali,

nasikia tayari wanasali wakati wa kanuni

ya Misa kumuombea Askofu Mkuu Yuda

Thadei Rwaichi, hawajafanya dhambi kwa Kumuombea, maana katika Misa

tunawaombea Maaskofu wote. Lakini kisheria ni kwamba tunapashwa kungoja mpaka apokelewe Jimboni na hivyo

anakuwa ni mtumishi katika Jimbo kuu la Dar es Salaam hapo kisheria tunamuweka katika hiyo sala katika Ekaristi Takatifu."

Alisisitiza na Kusema;

"Narudia tena, walioanza kusali

hawajafanya dhambi wasiende kuungama. Ila kisheria na Yesu alisema Mambo ya

Sheria... Sijui tufanyeje, Kisheria ni mpaka atakapo report hapa Jimboni ndipo

Mapadri mnalazimika kumtaja katika sala ya Ekaristi Takatifu."

Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alisema hayo kwa kina ili kutoa ufananuzi

zaidi jinsi taratibu za Kanisa

zinavyohitajika kufanyika.

Kanisa Katoliki ni Moja, Takatifu, Katoliki, La Mitume, La Kimisionari. Amina.

No comments:

Powered by Blogger.