WASIFU WA MAREHEMU PADRE UBALDUS KIDAVURI
A. ALIPOZALIWA NA KULELEWA
ยท Alizaliwa tarehe 13. 10.1961 katika parokia ya Kisangara Juu katika wilaya ya Mwanga, jimbo Katoliki la Same
ยท Wazazi wake ni Baba Francis Maliare na Mama Odilia Odilo
ยท Alipata Sakramenti ya Ubatizo tarehe 31.10.1961 katika parokia ya Kisangara Juu
ยท Alipata Sakramenti ya Kipaimara tarehe 31. 08.1974 katika parokia ya Kisangara Juu
B. ELIMU YAKE
ยท Alisoma shule ya Msingi Kiasangara Juu darasa la kwanza hadi la saba na kuhitimu tarehe 04.10.1975
ยท Alipata elimu ya Sekondari katika Seminari ya Mt. Petro Morogoro na kuhitimu Kidato cha nne tarehe 21/11/1980.
ยท Baadaye alijiunga na seminari ya Mt. Yakobo Kilema Moshi kwa ajili ya Masomo ya Kidato cha tano na sita ambapo alihitimu tarehe 7.4. 1983.
ยท Alijiunga na seminari Kuu ya Mtakatifu Bikira Maria wa Malaika Kibosho Moshi kwa ajili ya masomo ya Falsafa tangu tarehe 31 /7/1983 hadi tarehe 11/6/1985.
ยท Mwaka huo huo wa 1985 aliendelea na masomo ya Tauhidi katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga mpaka 1990.
ยท Alipata daraja la Ushemasi tarehe 18.6. 1992
ยท Alipata Daraja la Upadri tarehe 17/12/1992
C. UTUME WAKE JIMBONI
ยท Desemba 1992- Mlezi Dido Chuo cha Malezi
ยท Desemba 1992 Kaimu Paroko- Parokia ya Chanjale/ Kapelano Kisekibaha
ยท Mwaka 1993-1998 alikuwa paroko wa parokia ya Ugweno
ยท Mei โ Novemba 1998 alitumwa kusomea mawasiliano katika Chuo cha Uandishi wa Habari- Ndola Zambia
ยท 1998 -1999 Alikuwa paroko wa parokia ya Chabaru
D. UTUME WAKE KATIKA BARAZA LA MAASKOFU
ยท Aliteuliwa na Kamati ya Tendaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ( Permanent Council) tarehe 7.11.2003 kuwa mhariri mkuu wa Gazeti la Kiongozi, Mratibu wa programu ya radio na TV. Alianza kazi rasmi mwezi Desemba 2003 katika Idara ya Mawasiliano.
ยท Baadaye mwaka 2007 alitumwa huko Roma nchini Italia kujiendeleza katika fani ya Mawasiliano katika Chuo cha Msalaba Mtakatifu ambapo mwaka 2010 alihitimu shahada ya uzamili (Masters Degree) katika Mawasiliano. Wakati wa Masomo yake Roma alikuwa mhariri wa programu ya Kiswahili Radio Vatican 2007 mpaka 2009
ยท Baada ya masomo yake Roma alirudi jimboni Same na mwaka 2011 alitumwa kuwa paroko wa parokia ya Ugweno.
ยท Aliteuliwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tarehe 1. 7.2012 kuwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Walei na akateuliwa tena tarehe 1 Julai 2016 kuendelea na utume huo. Mpaka mauti yalipomkuta alikuwa anaendelea na utume huo.
E : UGONJWA WAKE:
Alikuwa akisumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo ambao ulisababisha kifo cha ghafla tarehe 13/04/2018
F: SHUKRANI
Baraza linashukuru kwa Mababa Askofu , mapdri na watawa na Wakristo mbali mbali ambao wameshiriki kwa njia mbali mbali kutoa faraja kwa Jumuiya ya Sekretariati tulipopatwa na msimba huu mzito.
No comments: