MASOMO YA MISA JUMANNE 21 NOVEMBA 2017 JUMA LA 33 LA MWAKA KUMBUKUMBU YA KUTOLEWA BIKIRA MARIA HEKALUNI.
SOMO 1:Zek.2:10-13
Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa, kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile,, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako. Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena. Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.
WIMBO WA KATIKATI
Lk. 1:46-55 (K) 46
(K) Mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu.
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
Na roho yangu imemfurahia Mungu,
Mwokozi wangu. (K)
Kwa kuwa ameutazama,
Unyonge wa mjakazi wake.
Kwa maana, tazama, tokea sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,
Na jina lake ni takatifu. (K)
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi
Kwa hao wanaomcha.
Amefanya nguvu kwa mkono wake;
Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao. (K)
Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;
Na wanyonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha mema,
Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. (K)
Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;
Ili kukumbuka rehema zake;
Kama alivyowaambia baba zetu,
Ibrahimu na uzao wake hata milele. (K)
INJILI:Lk.11:27-28
Yesu alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.

SHANGILIO
Lk. 1:28
Aleluya, aleluya,
Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Umebarikiwa katika wanawake.
Aleluya.

No comments: